Saturday, February 6, 2016

WALIMU WA ELIMU MAALUM NA WANAFUNZI WA ELIMU MAALUM WAKUTANE SHULENI





Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum anamhitaji mwalimu mwenye taaluma ya elimu maalum; pia mwalimu wa elimu maalum anamhitaji mwanafunzi mwenye mahitaji maalum. Ni mtegemeano wa aina yake.


Tanzania, kama nchi zingine duniani, ina wanafunzi wenye mahitaji maalum. Pia ni bahati iliyoje kuwa na vyuo vyenye kutoa elimu maalum kwa walimu ili kukidhi mahitaji maalum ya wanafunzi hao wenye mahitaji maalum.

Hata hivyo kuna kila dalili ya kushuka kwa huduma za elimu maalum nchini Tanzania. Walimu wengi wanaomaliza kozi za vyuo vya elimu maalum wamekuwa wakipangiwa shule za kawaida (normal schools) zenye watoto wasio na mahitaji maalum.

Kwa upande mwingine wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini wameendelea kuwepo mitaani bila kwenda shule kwa kigezo kuwa hakuna walimu wa kuwafundisha hawa watoto.

Elimu jumuishi bila mipango inaumiza wachache.


HOJA

Walimu wenye fani ya elimu maalum wapelekwe kwenye shule maalum za watoto wenye mahitaji maalum; sambamba ni hilo, pia kuanzishwe shule maalum kwa watoto hao kwenye maeneo yasiyo na shule hizo. Zipo wilaya nyingi zisizo na shule maalum, mfano halisi ni wilaya ya Mvomero, haina shule za viziwi na wasioona.


9 comments:

Sanga Fidelis said...

Kiukweli mimi hadi leo hii inaniuma sana kusomea Elimu maalumu halafu kupangwa shule ya kata ya kawaida. Nilitamani na nazid kutamani nipelekwe shule ya wanafunzi wenye ulemavu ili taaluma yangu itumike mahala pake husika

Philemon Sokime said...

Kiukweli hilo suala halijakaa sawa! Nakumbuka walimu wahitimu wa elimu walikuwa zaidi ya 400, lakini hata mmoja hakupelekwa shule maalum kwa makusudi! Kazi IPO!

Unknown said...

Shukulu umepata hata Kara wezio na degree zetu za special needs tuko mtaan

Unknown said...

Shukulu umepata hata Kara wezio na degree zetu za special needs tuko mtaan

Unknown said...

Hii ni hatari

Unknown said...

Au tusiisome hii coz

Unknown said...

Bado jamii ina uhitaji mkubwa pia was kupata elimu kuhusu watu wenye ulemavu ni dhahiri kwamba wazazi wengi wenye watoto wenye ulemavu wamekuwa wakitengwa na jamii kutokana na jamii kuwa na dhan potofu juu ya ulemavu ni kazi yetu wasomi katika kada hii kubuni njia zitakazoleta mabadiliko katika jamii ili kujenga jamii jumuishi.

Anonymous said...

Wadau msada special needs vyuo vina patikana wapi na wap

Anonymous said...

Vyuo vnapatkana wap