Thursday, December 25, 2014

‘Sera kuhusu walemavu zipo, hazitekelezwi’

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi yaUtafiti kuhusu Kupunguza Umaskini nchini (Repoa), Prof. Samwel Wangwe amesema sera zinazohusu watu wenye ulemavu zipo lakini hazitekelezwi.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupokea tafiti iliyohusu namna wenye ulemavu wanavyoshirikishwa kwenye programu za mifuko ya hifadhi za jamii, Profesa huyo aliitaka serikali kuanza utekelezaji wa sera hizo sasa.
“Matokeo ya stadi hii tuliyofanya tutayapeleka serikalini kwa ajili ya utekelezaji… tunaishauri namna bora na sahihi ya kutekeleza sera hizo kwa kuwa wenye ulemavu nao wanaweza kuchangia pato la taifa kwa shughuli mbalimbali wanazofanya,” alisema Profesa Wangwe.
Fredrick Msigala ni mwakilishi wa wenye ulemavu kutoka CCBRT aliyeshiriki kufanya stadi hiyo kwenye baadhi ya wilaya hapa nchini alisema ni vema wakashirikishwa kutunga na kutekeleza sera zinazowahusu.
“Stadi hii imeona ni kiasi gani programu na mifuko ya hifadhi za kijamii zinawasahau wenye kuanzia kwenye namna ya kuwahudumia mpaka miundombinu ambayo sio rafiki kwetu.
“Tunaitaka serikali sasa itushirikishe wenye ulemavu tuweze kutunga sera kwa sababu matatizo yetu hayawezi kusemewa na mtu asiye mlemavu tunazo changamoto nyingi na sisi ndiyo pekee tunaoweza kuzisema sio mtu mwingine.
Stadi hiyo ilifanyika kwenye wilaya za Nachingwe, Muheza na Mbeya Mjini kwa ufadhili wa GIZ wakishirikiana na Repoa.

MFUKO WA GEPF WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI




Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina akiongea na vyombo vya habari juu ya mipango ya Mfuko huo kutoa misaada kwa jamii hasa kwa wale wenye mahitaji kama walemavu wa ngozi (Albino) katika shule ya matumaini ya Jeshi la Wokovu iliyopo Kurasini



Mtoto Maria Mwingira akipokea msaada wa mafuta maalum ambayo hukinga ngozi yao wakati wa jua kali kutoka kwa Meneja Masoko wa GEPF, Bw. Aloyce 


Ntukamazina.Kijana Salum Iddi akitoa neno la shukurani kwa Mfuko wa GEPF 




Watu wenye ulemavu tutumie siku hii kutafakari vizuri


Katika sikukuu hizi watu wenye ulemavu tutaona mengi
1. Tutakirimiwa
2. Tutaonyeshwa upendo na wengi
3. Tutaonyeshwa kwenye vyombo vya habari kuwa watu wanatujali
4. Nasi tutafurahi sana!

Lakini katika yote hayo sisi watu wenye ulemavu tutafakari mahali tulikotoka, mahali tulipo na mahali tunakokwenda. Hii itatusaidia kujiwekea mikakati ya kuondokana na utegemezi na kupunguza dhana ya kujiita na kuitwa wanyonge.


Kuwa imara, katekeleze likupasalo, hakika utafanikiwa!

Nakutakia sikukuu njema ya Christmas! 

Tuesday, December 23, 2014

For sure! Disability isn't inability

When we write to the World about inclusive society we are actually searching for practical issues which were seen not applicable so some people in the past. These very burdened community for every kind of injustices are people with disabilities. They have, for a long time been isolated in many societal crucial issues.

We witness to all people around the world that, disability is not inability! If you don't help them don't block what they try to perform. It has been a tendency that our community systems put huge burdens to people with disabilities. These barriers are the ones that weaken the motivations and talents inherent with people with special needs. Let's give them the chance to think and act, let's consider them productive citizens, let's think differently over them, let's include them in all socio-political and economic affairs necessary for human beings. Yes! If you don't touch them productively, you then are advised not to hurt them! Leave them free!

Check this video clip to change your attitudes! 

Think differently! 

Sunday, December 21, 2014

Tunataja SEKOMU kwa elimu maalum



Kila ustaarabu katika historia ya maisha ya mwanadamu huwa na eneo ambalo umeanzia.
Katika historia ya Elimu Maalum kwa vyuo vikuu imeanzia SEKOMU. Nakumbuka topic ya "Advocacy for people with disabilities". Zipo nadharia mbalimbali zinazohusu ulemavu, mojawapo ni ile iitwayo "Social Disability" ambayo inadai kuwa duniani hakuna kitu kinachoitwa ulemavu wala mtu mwenye ulemavu bali ni tafsiri iliyoundwa kwenye jamii ili kuwabagua binadamu wengine. It is a social constructed concept!
Pia nakumbuka maneno ya Prof. Bagandanshwa kuwa katika utetezi wa haki za watu wenye ulemavu tunaambatanisha maana katika kila tukifanyacho katika utetezi huo (in every action we do for advocating people with disabilities there must be meaningful context attached to it).

Nakumbuka pia maneno ya rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akihutubia jumuia wa wana SEKOMU tarehe 9 July, 2014 alisema: "Sasa tunajua, tunapotakiwa kujua habari za elimu maalum tunawauliza watu wa SEKOMU". 

Ninaamini kuwa SEKOMU, mbali na taaluma zingine zinazotolewa hapo, kitaendelea kukumbukwa hasa kwa ajili ya elimu maalum.

Sherehe ya kuwapandisha vyeo ngazi ya uprofesa. 
Waliopandishwa vyeo ni Dr. Edward Bagandanshwa 
(wa kwanza kutoka kushoto, na Dr. Mbatia (wa tatu kutoka kushoto)

Stafu ya SEKOMU wakati wa hafla ya kuwapandisha 
vyeo kitaaluma Dr. Bagandanshwa na Dr. Mbatia kuwa profesa.
Ustaarabu huu mzuri wa Elimu Maalum kwa vyuo vikuu umeanzia SEKOMU, tunahitaji sasa kuueneza kwenye vyuo vikuu vingine nchini. Hii ni kwasababu, watu wenye mahitaji maalum ni wengi, wapo mijini na vijijini, wakubwa kwa wadogo. Tunahitaji kujenga jamii jumuishi ambayo kila mtu anathubutu kumjumuisha mwenzake.

Viva SEKOMU...

Saturday, December 20, 2014

Tanzania na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu & Mkataba wa Nyongeza (2006)


Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu duniani. Miongoni mwa haki za watu wenye ulemavu ni ile inayohusu elimu. Ibara ya 24 ya mkataba huu imeongelea kwa undani habari za elimu kwa watu wenye ulemavu. Tuusome huu mkataba kisha tujitathmini wenyewe kama taifa na kujiuliza swali moja tu; 
"Je, tumeweza kuitimiza hii haki ya watu wenye ulemavu kujipatia elimu yao ipasavyo?"



Ibara ya 24
Elimu

"1. Waliouridhia Mkataba huu, wanatambua haki za watu wenye ulemavu kupata elimu. Ili haki hii ipatikane bila ya ubaguzi na kwa misingi ya usawa wa fursa, Waliouridhia Mkataba, watahakikisha kuwepo kwa mfumo wa elimu jumuishi katika ngazi zote na mfumo wa ujifunzaji kwa maisha yote ukijielekeza kwenye:

(a) Uendelezaji kamili wa uwezo wa binadamu na uzingatiaji wa hadhi na kujithamini, kuimarisha hali ya kuheshimu haki za binadamu, uhuru wa kujiamulia na uanuwai miongoni mwa binadamu.

(b) Watu wenye ulemavu kujiendeleza kadri wawezavyo kihaiba, kivipawa na kiubunifu, kadhalika na uwezo wao kiakili na kimwili;

(c) Kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki ipasavyo katika jamii iliyo huru.

2. Ili haki hii ipatikane, Waliouridhia Mkataba huu watahakisha kwamba:

(a) Mfumo wa elimu hauwatengi watu wenye ulemavu na
kwamba watoto wenye ulemavu hawabaguliwi kwenye elimu ya msingi ambayo ni ya lazima au ile ya sekondari kwa misingi ya ulemavu;

(b) Watu wenye ulemavu wanaweza kuipata elimu ya msingi na ya sekondari katika mfumo jumuishi, bora na bila ya malipo kwa misingi ya usawa na wengine katika jamii waishimo.

(c) Marekebisho stahili yanafanyika kulingana na mahitaji binafsi;

(d) Watu wenye ulemavu wanapata usaidizi unaohitajika ndani ya mfumo wa elimu, ili kuwawezesha kuelimika vilivyo;

(e) Hatua za makusudi za kumuwezesha mtu binafsi mwenye ulemavu zinachukuliwa katika mazingira yanayomuwezesha kufikia upeo wa maendeleo ya kitaaluma na kijamii kama lilivyo lengo la ujumuishaji kamilifu;

3. Nchi zilzoridhia Mkataba huu, zitawawezesha watu wenye ulemavu kujifunza maishani na stadi za kimaendeleo katika jamii ili kurahisisha ushiriki wao ulio kamilifu katika nyanja ya elimu na kama wanajamii wengine. Ili kufikia lengo hili, Waliouridhia Mkataba huu watachukua hatua zinazofaa, zikijumuisha:

a) Kuwezesha mafunzo ya maandishi ya nukta nundu, maandishi mbadala na njia za kukuza mawimbi ya sauti na nyinginezo za kuboresha mawasiliano, mbinu kabilifu za ujongeaji, na kuwezesha huduma za makundi rika na ushauri;

b) Kuwezesha mafunzo ya lugha ya alama na kukuza utambulisho wa kiisimu wa jamii ya viziwi;

c) Kuhakikisha kwamba elimu kwa watu wenye ulemavu, hususan watoto wasioona, viziwi au viziwi wasioona, inatolewa kwa lugha, mfumo na njia sadifu za kimawasiliano, na katika mazingira yatakayotoa nafasi kubwa ya maendeleo kitaaluma na kijamii.

4. Ili kusaidia katika kuhakikisha upatikanaji wa haki hii, Waliouridhia Mkataba huu watachukua hatua madhubuti katika, kuajiri walimu, wakiwemo walimu wenye ulemavu, walio na utaalamu wa lugha ya alama na/au nukta nundu na pia kuwafundisha wataalamu na watumishi katika ngazi zote za elimu. Mafunzo kama hayo yatajumuisha mwamko kuhusu ulemavu na kutumia njia za kukuzia mawimbi ya sauti na zile mbadala kimawasiliano, mbinu na vifaa vya kimafunzo vitakavyowasaidia watu wenye ulemavu.

5. Waliouridhia Mkataba huu, watahakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapata elimu ya juu, mafunzo ya ufundi, elimu ya watu wazima na mafunzo wakati wote wa maisha yao bila ya ubaguzi wa aina yoyote na kuipata kwa misingi sawa na watu wengine. Ili kufikia hatua hii, Waliouridhia Mkataba huu watahakikisha kwamba marekebisho stahiki yanafanyika kwa ajili ya watu wenye ulemavu."

NB:
Elimu Jumuishi Tanzania bado ina kasoro kadhaa ambazo sote kwa pamoja kama taifa tunahitaji kuzirekebisha:
1. Upungufu wa walimu wenye utalamu wa elimu maalum
2. Upungufu na/au ukosefu wa vifaa saidizi kwa watoto wenye mahitaji maalum
3. Mtazamo juu ya ulemavu na watu wenye ulemavu bado haujaeleweka vizuri
4. Mazingira ya kielimu kwenye shule jumuishi si rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum


Thursday, December 18, 2014

Thank you Prude for your inclusion perspectives!


This girl lives in Venice, Italy. She is real working hard to create an inclusive society. Furthermore, she is aware that human beings are different from each other, and that each one needs (regardless of their ability differences) one or more assistance from his/her immediate person. These were her exact words as she passed on the Venice squares and unknowingly passed by a hearing impaired person.

"Feeling guilty, on the way home, passing along the bar i saw a man in his 40-50 staring and saying unclear words full of gesture to me, as i was rushing i just gave him a glance and didn't think he could be talking to me.Whilst contemplating what he was saying, i had a very powerful information in my brain telling me the man was indeed talking to you and he is dumb and uses sign language i felt so bad! I was hearing his words like an echo in my ears and the moves of his hands "sei bella" (you are beautiful), i was sad because i neither smiled nor showed appreciation to a person who is so pure, sincere and sweet. I am here in this world to make an inclusive society not exclusive world. I hope my reaction toward this man didn't make him feel its because of his condition i didn't pay attention to what he was saying. I will be walking on that square hoping to see him again! 


This is for you