Monday, August 26, 2013

MFAHAMU PENDO SIMON MWENYE UJUZI KIBAO


 Jina: Pendo Simon
 Ulemavu: Kiziwi
 Elimu: Shahada/Degree

Huyu hapa pichani ni dada mwenye fani mbalimbali ambazo zinamtosha kujitegemea kwenye maisha yake. Pia anaweza akaisaidia jamii kwa namna ambayo wengi wasingeweza kuifikiria. Pendo Simon anaweza, ni mthubutu na mchapa kazi kwa kutumia fani alizonazo.

Fani zake
      Ualimu wa elimu maalum
      Mchoraji wa katuni
      Designer (kama vile T-shirt designs)

Pendo Simon amewahi kufanyia kazi kwenye makampuni na asasi mbalimbali wakati akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Kila akipata likizo makampuni na taasisi mbalimbali zilimtafuta ili afanye kazi zao. Kwa sasa amemaliza elimu yake ya chuo kikuu na yuko kwenye kipindi cha kutafuta kazi ya kudumu kwa ajili ya maisha yake na familia yake.

Mtazamo Wangu

Kwa muda mrefu jamii zetu zimekuwa na ubaguzi kwenye eneo la ajira kwa watu wenye ulemavu; mbaya zaidi ni pale mtu mwenye ulemavu alipotazamwa kwa jicho lililokosa ujuzi wa kutathmini uwezo wa mtu. Namkumbuka rafiki yangu mwalimu asiyeona (visually impaired)- ambaye kwa sasa ni Lecturer, ana PhD. Siku aliyokwenda kuripoti kwenye kituo chake cha kwanza cha kazi alikataliwa na wanafunzi pamoja na mwalimu wa taaluma wa shule hiyo kukosa imani naye. Alijitambulisha kisha akawauliza mahali mwalimu wao alipoishia kufundisha. Alitumia dakika 15 kuwaonyesha namna anavyoweza kufundisha, kisha akaaga kuacha hilo darasa. Baada ya dakika 5 akiwa ofisini alifuatwa na wanafunzi, wakamwomba msamaha, halafu wakamtaka aendelee kufundisha.

Ukweli ni kwamba, watu wenye ulemavu wanapopata ujuzi fulani wanautumia kikamilifu, wanakuwa waaminifu kwa taaluma zao, wanakuwa na juhudi ambazo ni za juu sana. Jamii inatakiwa kufahamu kuwa watu wenye ulemavu wanachangia maendeleo kwa familia zao, kwa jamii  na kwa taifa  kiujumla.

Pia tukumbuke kuwa mtu mwenye ulemavu anaweza akafundishwa na kuumbiwa stadi anuai sambamba na watu wengine kwenye jamii zetu. Kwa mfano, tunao watu wenye ulemavu, mathalan wasioona, ni walimu kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu. Tena watu wenye ulemavu wana uwezo wa kufanya kazi ambazo tunahisi hawaziwezi. Kitu cha msingi ni kutengeneza mazingira jumuishi na yenye kufikika na watu wote kwenye jamii. Tujumuike kwa pamoja na kwa umoja ili kujenga nchi yetu bila kubaguana.

Tuwe ni watu wa kuona UWEZO wa mtu mwenye ulemavu mbali zaidi ya ULEMAVU alionao, yaani “SEEING ABILITY BEYOND DISABILITY” na tuwe na uwezo na wepesi wa kutathmini stadi za mtu mwenye ulemavu kabla ya kuhoji anachoshindwa kwa kuwa ulemavu si kukosa uwezo, yaani  "DISABILITY IS NOT INABILITY".

"Think Inclusively ~~~ Act Inclusively ~~~ Create an Inclusive Nation".

5 comments:

Anonymous said...

Watu wenye mahitaji maalum wanahitaji kupata ajira kama binadam wengine.

Anonymous said...

hata mi namkubali sana dada huyu yeye ni m2 wa tabasamu muda woote!

Philemon Sokime said...

Ni kweli kabisa, huyu dada ni mpambanaji sana. Nimewahi fanya naye kazi moja ya kuongea na watawala wetu, nilimkubali sana. Big up PENDO SIMON!

Anonymous said...

Asanteni jaman wapendwa I m happy to know that people support me

Philemon Sokime said...

Tuko pamoja@ Pendo