Mwl. Patrick Ngaillo (aliyekaa) akiwa katika kuandaa nukuu za somo la hesabu kwa kutumia mashine iitwayo "Perkins" kwa ajili ya watoto wasioona katika shule ya msingi ya watoto wasioona Buigiri- Dodoma.
Bwana Ngaillo ni mwl kutoka wilaya ya Sumawanga Vijijini katika shule ya msingi Sakalilo mkoani Rukwa. Kwa sasa yuko katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) kilichopo Lushoto mkoani Tanga.
Mwl Patrick Ngaillo anaamini kuwa kila mtoto ana haki ya kupata elimu bila kumbagua kutokana na hali yake. Hili ndilo lilomsukuma akaamua kusomea taaluma ya elimu maalum. Anaamini kupitia mpango wa elimu maalum utahakikisha kuwa hakuna mwanafunzi atakaeachwa katika mfumo wa elimu katika jamii zetu.
"Think Inclusively ~~~ Act Inclusively ~~~ Create an Inclusive Nation"
1 comment:
Hongera sana mwalimu Patrick Ngaillo kwa kujitoa kuhudumia wanafunzi wasioona. 'Pata elimu, tumikia kwa huruma'.
Post a Comment