Sunday, August 25, 2013

Nguvu ya Shule katika Kujenga Jamii Jumuishi


Mahubiri yakitafsiriwa kwa lugha ya alama                                    Wanafunzi wa shule ya Njombe                                                                                                                 Viziwi Wanamichezo wakihojiana                                                                                                             kwa lugha ya alama                                                                                                                                                        


Shule ni sehemu ambayo taifa linakuwa limeamua kupitishia sehemu ya utamaduni wake. Zipo tamaduni ambazo tunazipata kupitia uzoefu katika maisha ya kila siku.
Leo tuzungumzie utamaduni viziwi (deaf culture).

Katika jamii yoyote lazima utawakuta watu wa matabaka mbalimbali wakiwemo watu ambao ni viziwi (hearing impaired people). Kama binadamu wengine, watu viziwi wanahaki ya kuzifikia haki zao ikiwa ni pamoja na haki ya mawasiliano. Mawasiliano haya yanaweza fanyika mahali popote ambapo kuna mkusanyiko wa watu kuanzia idadi ya watu wawili. Kwa maana hii basi, maeneo yote ambayo kunakuwa na mkusanyiko wa watu lazima pawepo na huduma za kutafsiri lugha ya alama.

Maeneo ambayo yanaweza kutolewa huduma ya alama ya lugha ni pamoja na nyumba za ibada (kanisani na msikitini), shuleni, hospitali, benki, hotelini, na hata maeneo ya sokoni na maeneo mengine mengi.

Lugha ya alama inatakiwa kutambuliwa kama lugha rasmi ya Taifa la Tanzania sambamba na lugha zilizoteuliwa kutumika nchini. Ipo mifano ya nchi za Afrika ya mashariki ambazo zinaitambua lugha ya alama katika katiba zao. Mfano wa nchi hizo ni Uganda, Rwanda na Kenya.


Picha ya hapa juu ni ya mwalimu Frank Mkocha ambaye kwa sasa anasoma chuo kikuu cha SEKOMU. Serikali inatakiwa kuhakikisha walimu kama walioamua kusomea elimu maalu wanapewa motisha inayolingana na maamuzi magumu waliyoyachukua ili kuleta usawa katika taifa hili la Tanzania.





Pichani juu: Kikao kikiendeshwa huku watu viziwi wakipata huduma ya kutafsiriwa kwa lugha ya alama



Picha hizi hapa juu zinaonyesha alama za herufi kuanzia A-Z


Picha hizi hapa juu zinaonyesha alama za namba kuanzia 1-10




Hii  picha hapa juu ni ya watu wa Marekani wakionyesha alama ya kumpongeza mwenzao kwenye kumbukumbu yake ya kuzaliwa (birthday wishes). Wamarekani wana usemi wao wa "No One Left Behind". Kwa usemi huu kila mtoto anayezaliwa akiwa na ulemavu wowote lazima aishi na kufurahia maisha kama wengine kwa gharama za serikali. Italia wanasema ukiruhusu mtoto azaliwe lazima aishi, wao kwa mtoto aliyezaliwa akiwa na ulemavu anatengewa EURO 400 pamoja na huduma zingine ikiwa ni pamoja na elimu bure. Tanzania nasi twaweza fikiria huduma kama hizi kwa watu wenye mahitaji maalum.


Hitimisho

Kama taifa moja, lenye umoja, lenye kupenda watu wake wawe wamoja; tunahitaji kuhakikisha kuwa mfumo wetu wa elimu, ambako tumeamua sehemu fulani ya utamaduni wetu upitie huko iimarishwe zaidi ili kujenga taifa imara zaidi. Tujiwekee utaratibu wa kuwawezesha watoto wetu kujifunza lugha ya alama kuanzia shule za msingi hadi kufikia elimu ya chuo kikuu. Kama nilivyotangulia kusema kuwa mawasiliano ni haki ya msingi ya binadamu awaye yote, hivyo kama taifa tunatakiwa tujenge msingi imara wa wa lugha ya alama.



"Think Inclusively, Act Inclusively ~~~ Create an Inclusive Nation"




No comments: