Wednesday, September 18, 2013

Elimu Maalum huenda mbali zaidi ya darasani




Elimu Maalum: 


Hii ni taaluma ambayo mtu husomea, hususan, ualimu, ambapo hulenga kutoa taaluma na ujuzi maalum kwa makundi maalum kwenye jamii ili yaweze kuzifikia huduma mbalimbali kwenye jamii kama vile kupata elimu, kupata ajira, nk. Makundi haya maalum mfano wake ni watu wenye aina mbalimbali za ulemavu, watoto yatima, jamii za wafugaji na watoto wa mtaani. Ni wajibu wa kila taifa kuandaa sera nzuri zenye kutimiza mahitaji ya wanajamii wake.
Nchi yeyote na jamii yeyote ile lazima utawakuta watu wenye mahitaji maalum, na ambao kwa namna moja ama nyingine lazima lazima iwepo njia mbadala ya kuwapatia mahitaji kutokana na asili ya mahitaji yao. Hapa ndipo panaonekana umuhimu wa elimu maalum. Na kwa kuwa sheria na tamaduni za binadamu zinaonyesha kuwa kiumbe yeyote aliyezaliwa na/au kutokana na binadamu lazima aheshimiwe kama binadamu. Na pia katika makubaliano mbalimbali ya kimataifa kama vile Salamanca, Haki za binadamu za Umoja wa mataifa na mengine mengi yameainisha haki za msingi za watu wenye mahitaji maalum.





Mwl Rose Yona akiwasiliana na mwanafunzi kiziwi kwa lugha ya alama ktk shule ya viziwi Mwanga mkoani Kilimanjaro.


Mwl Fanuel Mwakanosya akiwa ktk maandalizi ya kufundisha. Anatumia kifaa kiitwacho Perkins, mashine ambayo huweka maandishi ktk mfumo wa nukta nundu.

Mwl Magreth Msuya akitumia Perkins kuandaa nukuu za somo kwa wanafunzi wasioona wa shule ya msingi ya wasioona Buigiri mkoani Dodoma.

Mwl Magreth Msuya akimwezesha mwanafunzi wa darasa la sita somo la hesabu ktk shule ya msingi Buigiri.


Walimu Charles Kibugi (kushoto) na Ernest Ezron (kulia) wakiwa wanawaongoza wanafunzi wa darasa la kwanza kuelekea darasani. Elimu maalum haiishii darasani tu, huenda zaidi kuelekea shughuli zingine ktk maisha. Humwezesha mwalimu na yeyote mwenye kusoma taaluma ya elimu maalum kupata saikolojia ya kuweza kushirikiana na makundi anuai yaliyoko kwenye jamii zetu. Inawezesha mtu kupata stadi za maisha ya kila namna, uvumilivu, upendo na wakati mwingine kufanya kazi kwa kujitolea.

Hawa ni walimu waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo kutoka SEKOMU. Walio pamoja nao ni pamoja wakaguzi wa elimu shule za msingi wa kanda na wizarani, walimu wenyeji pamoja na wazee waanzilishi wa shule hiyo miaka ya 1950. Anayeonekana katikati (waliosimama), mwenye shati jeupe na miwani ni mwl mkuu wa shule ya msingi ya wasioona Buigiri, ndugu Sylivanus Hosea. Yeye pia ni mwalimu asiyeona (Blind). Hapa tunaweza kuona kuwa watu wenye ulemavu wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii zetu. Pia jamii inaweza kukumbushwa kuwa ulemavu si kukosa uwezo (Disability isn't inability).



Fikiri kijumuishi ~~~ Tenda kijumuishi ~~~ Jenga Taifa jumuishi.

8 comments:

Anonymous said...

I like it! Kweli elimu maalumu inahitajika ktk jamii yetu Kwan hawajui maana ya ulemavu so it us our responsibility to educate our society! Thank u admin Sokime for u a information and for u a heart to educate the society

Philemon Sokime said...

Thank you too@anonymous

Anonymous said...

elimu maalumu yahitajika zaidi kwa waalimu woote wa shule zoote kwani wenye mahitaji niwengi miongoni mwe2. Asante sana Bro kwa makala ii@By Mwanabusi

Philemon Sokime said...

Nashukuru kaka. Pamoja sana! @Paschal

Anonymous said...

Pamoja sana mkuu,Elimu maalum ni zaidi ya darasani,hata katika mikutano ya wanajamii na shughuli za kimaendeleo ya jamii,RAI:Waalimu na wanataaluma hii ya Elimu maalum,tutoe Elimu hasa kwa Wazazi pamoja na jamii inayotuzunguka,ili wajue nini maana ya Elimu maalum,umhimu wake,pamoja faida yake kwa jamii. Haki Sawa Kwa Kila Binadamu. From Ole Tisho.C

Unknown said...

Hii nimeipenda sana hii elimu maalumu maana Kuna jamii ambayo huwa haiwajali watoto kuwapatia elimu hususa ni jamii ya wafugaji watoto wanalelewa katika mazingira ya kuchunga tangu akiwa mtoto kwahiyo mtoto anakuja kukuwa hajui hata nini maana ya umuhimu wa elimu

Unknown said...

Ndio kabisa elimu maalum inatakiwa itolewe

Unknown said...

Nipo katika process ya kusoma ualimu wa Elimu hii ili nifanye kitu kwa ajili ya jamii yeyote itakayokuwa na uhitaji maalumu kulingana na kile nitakachokua nimejifunza, ahsante admin kwa Kuni inspire.