Sunday, September 14, 2014

Mzazi tambua namna ya kupunguza Athari Za Ulemavu Aina ya "Club Foot" kwa mwanao


Club Foot ni nini?
Hii ni aina ya ulemavu utokanao na matatizo ya mifupa ambapo kunakuwa na mkao usio wa kawaida wa unyayo wa mguu (unusual position of the foot).
Dalili za kuwa na “Club Foot”
1. Unyayo waweza kuwa mdogo kuliko ilivyo kawaida
2. Unyayo unaweza kuinamia chini (kutembelea vidole)
3. Mguu (unyayo) unaweza kuelekea ndani (turn in)
4. Ugumu wa kuvaa viatu
5. Ugumu wa kushiriki michezo itumiayo miguu (kwa watoto wakubwa)

Ulemavu huu mtu anapata wakati gani?
Club Foot nyingi ni za kuzaliwa (Congenitally Acquired), na nyingine hutokea wakati mtoto amezaliwa katika hatua yoyote ya makuzi ambayo husababishwa na vigezo vya kimazingira tu (environmental effects).
Ingawa Club Foot kwa watoto haina maumivu, lakini taratibu za kitabibu zianze mapema mara mtoto azaliwapo ili kupunguza athali zake kwa maisha ya kujitegemea baadae. Club Foot inaweza kusababisha matatizo mbalimbali kadri mtoto anavyoendelea kukua, lakini matibabu ya mapema humwezesha mtoto kuendesha maisha yake ya kawaida bila kuhitaji msaada.
Nini husababisha mtoto kupata “Club Foot”?
1. Mkao wa mtoto awapo kwenye tumbo la mama yake (kabla ya kuzaliwa).
2. Mchanganyiko wa athari za kiurithi (genetic factors) na za kimazingira (environmental factors) ambazo kwa sehemu kubwa haziwezi kubainishwa kwa urahisi.
Athari kuu za “Club Foot” kwa maisha ya mtoto
Uwepo wa “Club Foot” kwa mtoto kunaweza pelekea matatizo mengine kama vile mfumo wa fahamu kupungua ufanisi wake, ufanisi wa misuli mwilini hupungua; na pia mfumo wa mifupa nao hupungua ufanisi wake kwa maisha ya mtoto.
Ushauri
1. Wamama wajawazito wahudhurie kliniki kwa wakati ili kupata maelekezo muhimu kwa makuzi sahihi ya mtoto awapo tumboni.
2. Wazazi wajawazito wafanye mazoezi ya mara kwa mara (asubuhi na jioni) ili wawawezeshe watoto wao tumboni kujiweka sawa (to make self adjustments in the womb)
3. Mara mtoto akizaliwa na uonapo dalili dhahili za kuwepo kwa ulemavu wa “Club Foot” wahi kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe ili upate ushauri wa kupunguza athari za ulemavu huu.
4. Kwa vile “Club Foot” ni moja ya ulemavu utokanao na matatizo ya mifupa; hivyo ni vema kama wana ndoa wakashirikiana kwa karibu ili kuwezesha mtoto aliye tumboni kupata virutubisho sahihi vya kujenga mifupa. Pata ushauri wa kitaalam wa lishe.

Mtoto mwenye Club Foot

Upatapo elimu hii mshirikishe na mwenzako kwa ustawi wa familia zetu.




2 comments:

Anonymous said...

Hii elimu juu ya ulemavu inahitajika sana!

Anonymous said...

tunakushukuru endelea kutuelimisha!